Siku moja mwalimu wa sayansi aliingia darasani na kuchora picha ya moyo ubaoni,kwa kuwa hakuwa mchoraji mzuri ikabidi awaulize wanafunzi wake;
Mwalimu;Hebu niambieni ni picha ya nini hiyo ubaoni??
Wanafunzi;(kwa pamoja),ni picha ya MATAKO mwalimu.
Mwalimu;(Uku kachukia),eti john hiyo picha ubaoni ni ya nini?
John;Ni picha ya matako mwalimu;
Mwalimu akatoka uku akiwa kafura hasira hadi kwa mwalimu mkuu,akamweleza kuwa watoto wanaleta mzaha wakati yeye anafundisha.Mkuu wa shule pamoja na mwalimu wa sayansi wakaondoka pamoja hadi darasani;
Mkuu wa shule;Enhee,mwalimu hawa watoto unasema wanaleta matatizo gani??
Mwalimu;Nilikuwa nawauliza hiyo picha ubaoni wakawa wananidhihaki,
Mkuu wa shule;(uku akiiangalia picha kwa hasira),haya nyie watoto hebu niambieni nani kachora picha ya MATAKO ubaoni. kabla sijawatembezea fimbo sasa ivi?
Wanafunzi;(kwa pamoja),MWALIMU WA SAYANSI NDIO KACHORA.