Jamaa alienda kutoa posa kwa nyumbani kwa wazazi wa mwanamke,alivofika mambo yalikuwa kama ifuatavyo;
BABA MKWE;Mbona unaongea na sisi uku unatafuna big g
JAMAA;Samahani,ninatafuna ili nitoe harufu ya konyangi niliyokunywa
MAMA MKWE;Heeeh..unakunywa pombe??
JAMAA;Ndio,nilijifunza kipindi nilipo acha kuvuta bangi
BABA MKWE;Ulishawahi kuvuta bangi??
JAMAA;Ndio,kipindi nilipokuwa gerezani
MAMA MKWE;Na gerezani  kumbe umeshawahi  kwenda?
JAMAA;Ndio nilienda miaka kumi iliyopita kwa kosa la kuua
BABA MKWE;Kumbe wewe ni muuaj?
MAMA MKWE:Kwa nini uliamua kuua??
JAMAA;Niliua wazazi wa binti niliyekuwa nampenda kwa sababu hawakutaka nioe binti yao,ila kwa bahati mbaya binti alijinyonga wakati niko gerezani.Sasa nilivotoka ndio nikampenda binti yenu.
BABA MKWE;Ooooh..kumbe ndo ivo,haina shida baba,binti yetu yule mchukue hatuitaji hata posa wala mali yako.