- Acha tabia ya kupiga punyeto;Tabia au mazoea ya kupiga punyeto yanamadhara makubwa sana wakati wa tendo la ndoa.Mwili wa mwanaume aliezoea kupiga punyeto au kujichua huathirika katika mfumo wa uzazi hasa misuri inayo ruhusu usambazaji wa damu kwenye uume kulegea na mwanaume kushindwa kusimamisha uume wake sawa sawa(90 DEGREE),au kusababisha mwanaume kuwahi kufika kileleni na kushindwa kuendelea na mchezo.
- Kula chakula bora;Chakula bora ni dawa na ni siri kubwa ya kuwezesha kuwa na afya bora na uwezo mkubwa wa kulishinda tatizo la nguvu za kiume kama wengi tunavoamini.Kila siku hakikisha unapata chakula bora kwa ajili ya kuwezesha mwili wako kuwa wenye afya njema na kuwa na uwezo wa kufanya kazi kifanisi hasa katika tendo la ndoa.Pata matunda na chakula cha kutosha kwa muda unaostahili.
- Mazoezi;Mazoezi pia ni siri kubwa ya kuondokana na tatizo la nguvu za kiume.Hapa siongelei kunyanyua vyuma,bali ni yale mazoezi ya kawaida yanayosaidia kujenga mwili.Mazoezi kama kukimbia,kuruka kamba,kuruka kichura,kupiga push-up.Pata mda wa kufanya mazoezi kila siku kwa dakika 20 na utaona mabadiliko katika mwili wako wakati wa tendo la ndoa.
- Pata muda wa kutosha wa kupumzika;Siri nyingine ni muda wa kutosha wa kupumzika.Tenga muda wa kupumzika baada ya kazi zako.Hakikisha unapata angalau masaa mawili kila siku ya kulala kama inawezekana.Mwili hufanya kazi kifanisi zaidi pindi mtu akiwa amepumzika,
- Zingatia elimu ya afya bora;Hapa nazungumzia elimu yeyote inayohusika na afya yako ni muhimu kuzingatia ili kujiweka katika mazingira mazuri zaidi,weka mazoea ya kwenda hospitalini kufanya uchunguzi wa mwili wako usisubiri mpaka uumwe ndo uende hospitali
Kwa kufanya hayo machache nina uhakika tatizo la nguvu za kiume litakuwa ni hadithi katika maisha yako,Nina imani utamsaidian na mwingine juu ya tatizo hili lenye kuleta aibu mbele ya mwezi wako na kujiona sio mwanaume kamili.Mpaka wakati mwingine tena kwaherini