Tcra -Tanzania


Baada ya mke kumtafuta mumuwe kwenye cm tangu jana usiku hapatikani akamua akirudi amuwekee mnuno.
Baada mume kuingia:
Mume: Baby mambo vipi?
Mke: Kimya ??
Mume: Nmekumisije.
Mke: Kimya ??
Mume: Chakula vipi?
Mke: Kimya ??
Mume: Uko sawa kweli?
Mke: Kimya ??
Baada ya kuona hakuna jibu akaanza akashika kichwa, "TCRA sasa huku mmefika mbali mmezima simu yangu tangu jana mmeona haitoshi naona mmeamua kumzima hadi mke wangu?"
Mke ilibidi aangue kicheko tu