Je wajua aina za marafiki ulionao?.
-Zifuatazo ni aina ya marafiki wanaokuzunguka.
§ Wanaotafuta umaarufu kupitia wewe;
Kundi la watu wa aina hii wanapenda kuwa na urafiki na wewe kwa sababu wanalengo la kutengeneza majina yao kupitia sifa zako katika jamii inayokuzunguka.Mara nyingi watu hawa hupenda kushinda na wewe wakati mda wote na kila tukio unalolifanya hupenda kuonekana nay eye alishiriki ili mradi jamii wajue uwepo wake na aweze kutimiza lengo lake kubwa alilo azimia.Mara nyingi watu hawa ni wale ambao wanajua vizuri kitu kikubwa kinachokupa heshima katika jamii inayokuzunguka hivo na yeye kuhakikisha anatumia hiyo hiyo sifa uliyonayo ili kutengeneza jina lake katika jamii na kutumia urafiki kama njia kuu ya kuwa karibu na wewe.
· Wanaokuwa na wewe kwa sababu unawasaidia kwenye matatizo yao
Aina ya marafiki hawa ni wale wanaokuwa na wewe kwa sababu unawasaidia pindi wanapopata matatizo.Watu hawa pindi ukiwasaidia matatizo yao hujitenga na kuwa mbali na wewe lakini pindi akipata tena matatizo hujisogeza karibu ili kujenga urafiki wa kinafki kama mwamvuli wa kutatua matatizo yake.Marafiki wa aina hii hauwezi tegemea msaada wowote kutoka kwake.
· · Marafiki wa kweli;
Huyu ni rafiki Yule ambaye anakuwa na wewe wakati wa matatizo.Kwa nini nimesema wakati wa matatizo na sio war aha?.Hi ni kwa sababu wakati war aha ni ngumu sana kujua yupi ni rafiki wa kweli na yupi ni mwigizaji.Pindi unapopata matatizo ndio kipindi unapojua yupi ni rafiki wa kweli lakini sio kipindi uko kwenye raha.Rafiki wa kweli hapendi kukuona wewe ukiwa kwenye shida tene shida inayokufanya muda wote ukose furaha,muda wote kushinda unawaza.Rafiki wa kweli yupo tayari kujitoa yeye muhanga ili kukusaidia rafiki yake.Rafiki wa kweli anakuwa kama kivuli chako.Ni rafiki ambaye hapendi kukukwaza kwa jambo lolote na hukueleza ukweli pindi unapofanya mambo vibaya.
· · Marafiki kigeugeu;
Hii ni aina ya marafiki wanaokuwa na wewe wakati wa raha peke ake.Marafiki hawa hawa tofautiani sana marafiki wanaokuwa na wewe kwa sababu unawasaidia shida zao .Tofauti yao kubwa ni kwamba hawa huwa na wewe ukiwa katika hali nzuri ya kiuchumi na kukuongelea vibaya kwa watu wengine pindi ukishuka kiuchumi.Marafiki wa aina hii huwa hupenda kukaa na kumuongelea mtu mwingine.Njia kuu anayoitumia kuanzisha urafiki na wewe ni kwa njia ya kumsema mtu mwingine ili wewe ufurahi lakini pindi na wewe ukipata matatizo rafiki huyu hukuacha na wewe kuwa stori mpya kwa rafiki wake mpya.
· · Marafiki wachunguzi;
Hawa ni marafiki wale ambao huchunguza maisha yako unaishije ili waweze kujua wewe ni mtu wa aina gani.Marafiki hawa ni wabaya sana mana huwa wanakufuatilia kwa siri sana mambo yako nyeti na kuyaanika kwa jamii ili uhadhirike.Aina ya marafiki ni sawa na mtu anaekuchekea usoni uku moyoni anawaza akuue kwa kutumia njia ipi.
Naimani mpaka hapa unaweza ukawachambua aina ya marafiki ulionao.
Kuna aina nyingi sana za marafiki wanaokuzunguka katika jamii ila kwa leo naishia hapa.
************************************************************************************