Inaweza isiwahusu vijana peke yao lakini kwa kutambua wingi wa rika letu nimeamua kuwalenga wao ili kuwapa mbinu za kuweza kuwasaidia kujikomboa kimaisha. Hapa chini kuna muongozo wa kumfanya kijana afanikiwe kimaisha.
UNACHOAMINI
UNACHOAMINI
Njia ya kwanza ya kijana kujikomboa inaanzia kwenye kile anachoamini katika maisha yake. Katika hali ya kawaida mwanzo wa imani ya mwanadamu hutoka kwa wazazi wake na wakati mwingine mazingira atakayokulia.
Hali iko hivyo kwenye njia hii ya kwanza ya kijana kuelekea kwenye mafanikio. Wengi tumezaliwa na kurithishwa imani ya kutofanikiwa. Wazazi wetu walitulea kwa kutuambia maisha ni magumu, hatuwezi kufanikiwa, sisi ni masikini, duni na maneno kama hayo ya kukatisha tamaa.
Mawazo ya vijana wengi leo yanaamini kuwa, umasikini ni mzigo mkubwa usiokuwa na ufumbuzi. Kitaalamu mtu anapokuwa na mawazo ya kutokufanikiwa hawezi kufanikiwa kwa sababu mafanikio huhitaji nguvu na nguvu za mwili haziwezi kujitokeza kama hazikuvutwa kufanya kazi.
Kwa msingi huo, ili mtu aweze kufanikiwa lazima mawazo yake yakubali kuwa mafanikio ni sehemu ya lazima katika maisha. Jambo hili haliwezi kutokea mpaka kijana mwenyewe aliyelelewa kwenye mawazo ya kushindwa apigane vita na mawazo ya kutofanikiwa na kuyashinda.
Njia pekee ya kujikomboa na mawazo mgando ni kufuta na kupuuza kauli zote ulizoambiwa na mtu yeyote kuhusu maisha magumu na kuanza kuamini kuwa, maendeleo ni ngumu kuyafikia.
Siri kubwa ya mafanikio ni kujituma.Hamna maisha mazuri bila kujishughulisha na kitu chochote au kazi yeyote na tena kazi ambazo ni halali.Hakikisha kwenye shughuli zako unazifanya kwa ufanisi mkubwa na hata kuongeza muda wa ziada ili kuboresha kazi zako ili kuweza kuvuta wateja wa kutosha.Tumia kitega uchumi chako kufanikiwa kwenye maisha kwa kujifunza njia mbali mbali unaweza ukazifanya ili kuzidi kuboresha biashara yako na mwishoni mafanikio hupatikana lakini yote ni kwa sababu ya juhudi zako.
Mahusiano yako na watu wanaokuzunguka ni daraja lililopo kati yako na mafanikio yako.Huwezi kufanikiwa katika shughuli zako kama mahusiano yako na watu wanaokuzunguka sio mazuri.Jamii au watu wanaokuzunguka ndio wateja wako wakubwa katika shughuli zako kwa hiyo pindi mahusiano yako yakiwa mabaya na watu hao,shughuli zako za kiuchumi nazo zitakuendea vibaya kwa kuwa umewapoteza watu ambao ndio wateja wako wakubwa.