JE WAJUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATI YA ELIMU YA MTOTO NA FAMILIA?

Habari za saizi ndugu zangu,na imani, u-mzima wa afya tele kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu aliye juu.Leo katika safu hii nitaongelea namna au jinsi familia inaweza kuleta changamoto au kuwa tatizo kwa elimu ya mtoto.Vifuatavyo ni baadhi ya vipengele hivyo;-
v  UGOMVI WA WAZAZI WA MARA KWA MARA
Ugomvi baina ya wazazi huwa ni tatizo kubwa linalopelekea changamoto nyingi katika elimu ya mtoto ambazo hupelekea kushindwa kufanya vizuri katika masomo yake.Hii ni kutokana na mtoto kutumia muda mwingi kufikiria kwa nini wazazi wake wanagombana mara kwa mara na kushindwa kufikiria masomo yake vizuri.
v   UKOSEFU WA MSAADA KUTOKA KWA WAZAZI
Vile vile,asilimia kubwa ya familia zetu wazazi kutojali maendeleo ya mtoto juu ya masomo yake.Mtoto anabaki kuwa ndio mtu pekee wa kujiongoza mwenyewe katika masomo yake kwa asilimia kubwa uku asilimia ndogo inayobaki kuachiwa walimu wake ambaye hubakia kuwa mbeba lawama mkubwa pindi matokeo ya mtoto yanapokuwa mabaya.
v  MAISHA DUNI KATIKA FAMILIA
Hii kwa asilimia 90 huchangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa mtoto katika masomo yake.Mtoto kutumia mda mwingi kutafuta namna ya kuishi kuliko kufikiria masomo yake,kwa mfano;watoto wanao-okota vyuma chakavu,watoto wanao-okota makopo ya maji.Pia tunaona jinsi wanachuo wanaotokea familia duni wanavyopata shida chuoni kwa kukosa mikopo ya elimu ya juu ambayo hupelekea kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika masomo yao.

Ø  Kwa leo naomba niishie hapa,mpaka wakati mwingine tena katika mada nyingine.
                                        ASANTENI
******************************************************************************