DARE-ES-SAALAM KWA HAPA TUTAWEZA

Habari ya saizi ndugu msomaji wa blogu hii  Tanzania yangu,leo nimekuja na wazo ambalo nimeona linaweza likatatua hili tatizo la uchafu katika jiji la dar-e-saalam.Ukilinganisha na majiji mengine nchini Tanzania,dar-e-saalam ni jiji linaloongoza kwa uchafu hii ni kutokana na wingi wa watu katika jiji hili.Kwa kutumia njia zifuatazo kwa asilimia 20 tunaweza kupunguza uchafu katika jiji hili la dar-es-saalam;

1.Kuwepo kwa pipa la takataka kila baada ya mita 500
2.Kuwepo kwa mashimo ya taka kwa kila kitongoji ili kuzuia watu kutupa taka za nyumbani ovyo kama vile;-maganda ya viazi,maganda ya nyanya,mabaki ya chakula,n.k
3.Kuwepo na sheria kali zitakazoambatana na hatua kali za kisheria juu ya utunzaji wa mazingira
4.Kuwepo kwa magari maalumu kwa ajili ya kukusanya takataka na kupeleka sehemu ya kuchomea
5.Kila mwananchi kusimamia jukumu la kuzuia taka zisizo za lazima mfano;-kadi za vocha zilizotumiaka,maganda ya pipi,makopo ya maji,n.k

Kwa kufanya hivi kwa jiji la dare-e-saalam litapunguza uchafu ambao umekuwa kero kubwa.Napenda kupongeza baadhi ya miji kama Arusha na Moshi kwa usafi wanaouonyesha kila siku.Naamini  hata dare-e-saalam tunaweza.Asanteni