Mambo vipi vijana wenzangu,natumaini mko powa na mnaendelea vizuri na shughuli zenuza kila siku za kujenga nchi.Katika jukwaa letu leo nina mada inayosema “AKILI YAKO NDIO AJIRA YAKO”.
Kwa pamoja nadhani tunatambua jinsi maisha yanavyokuwa na changamoto kubwa kama hauna shughul yeyote ya kufanya ili kukuwezesha kupata mkate wa kila siku.Leo nataka kuelezea jinsi kijana mwenzangu unaweza kujikomboa katika umaskini kwa kutumia MALIASILI zinazokuzunguka bila kusubiri kuajiliwa kama wengi wetu tulivozoea.
Kwa kawaida binadamu tumezoea kuishi kwa mazoea,tumezoea kudharau vitu vidogovidogo bila kujua vinaweza kukusaidia kutuweka katika hali nzuri ya kiuchumi.Tumesahau ule usemi unaosema “HABA NA HABA HUJAZA KIBABA”.
Tatizo ni je nifanye ni njia zipi nitumie ili niweze kufaidika na mali asili zinazonizunguka ili kujiinua kiuchumi?
**ulishawahi kaa na kujiuliza lini utakuja kuwa na fedha nyingi bila kutegemea ajira?????***
Kama uliwahi kufikiria kupata fedha bila kutegemea ajira basi naimani kubwa uliwaza ni namna gani au njia gani utazitumia kupata hizo fedha kwa kutumia AKILI ambazo mwenyezi mungu katupatia,kwa kuweka mbali mawazo ya kupata fedha kwa njia ambazo sio halali
Kwa njia zifuatazo nina imani ukitumia vizuri mali asili zinazokuzunguka utaweza kujijengea ajira nzuri ambayo hautahitaji kuajiliwa badala yake wewe ukaanza kutoa ajira kwa wengine;
· Kama upo sehemu ambayo unauwezo wa kupata eneo la kulima unaweza ukaanzisha biashara ya mboga mboga.Biashara inahitaji mtaji mdogo na inachukua mda kidogo katika hatua zamwanzo kuanzia, ulimaji, umwagaji wa mbegu mbalimbali kama mchicha,maboga,kabeji,n.k k hadi pale mboga zitakapokuwa tayari kwa matumizi.Lakini pindi biashara hii itakaposhamili matokeo yake huwa makubwa tofauti na tunavoichukulia kwa kuongea.Na ni biashara unayoweza kuifanya kwa mda wako wa ziada.
· Biashara ya tofali;Vilevile ni biashara ambayo hudharaulika sana lakini ni biashara ambayo inafaida kubwa sana na mtaji wake ni nguvu zako na mda wako.Biashara ambayo hutegemea zaid mali asili ya ardhi ,misitu pamoja na maji.Pindi ukishamaliza kufyatua tofali huzisubiri kukauka na baadae kuzichoma ili kupunguza uzito na kuongeza uimara wake.Ni biashara ambayo inaweza kufanywa na kukindi cha vijana kwa kushirikiana pamoja na kujionea matokeo yake.
· Biashara ya mkaa;Mkaa umekuwa ukipanda siku hadi siku hii ni kutokana na kuongezeka kwa matumizi yake kwa sababu ya ongezeko kubwa la watu.Biashara hii inahitaji mda na nguvu za mwendeshaji,ni biashara inafaida kubwa sana nah ii ni kutokana na matumizi ya mkaa yalivomuhimu katika jamii zetu.Na ni biashara ambayo huweza kufanya na kikundi cha watu na kupata mafanikio makubwa
· Biashara ya mazao;Biashara hii hutokana na mali asili ya ardhi,lakini ni biashara inayohitaji mtaji kwa mtu anaetaka kuifanya.Kwa mkulima ataitaji mbolea,dawa,pamoja na pembejeo nyingine kwa ajili ya kilimo cha kisasa,na kwa wanunuzi watahitaji mtaji mkubwa kwa ajili ya kununua mazao kwa wakulima na kuyasafirisha sehemu mbalimbali kwa mtumiaji wa mwisho.
Siku zote huwa naamini AKILI YAKO ndio AJIRA YAKO.,tunaweza kuendelea kiuchumi bila kutegemea kuajiliwa.Na pia tuache kutumia njia za mkato ili kutaka kupata mafanikio ya haraka kama vile kutapeli,kuiba,n.k, kwa maana siku zote njia za mkato huwa zina athari zake.Hivyo nawaomba vijana wenzangu tuwe na mitazamo chanya juu ya maisha yetu na juu ya njia zetu tunazozitumai kutafuta riziki zetu za kila siku
Mpaka wakati mwingine tena,kwa herini.