Simba na jamaa
Baada ya maisha magumu jamaa kaenda kuomba kazi hifadhi ya wanyama,alipofika wakamwambia kazi ambayo wanaweza kumpa ni kazi ya yeye kujifanya sokwe pindi wanapokuja watalii.Kutokana na maisha magumu jamaa akakubali bhasi akakabidhiwa ngozi ya sokwe ili aivae.Siku walipokuja watalii banda la sokwe likawekwa juu ya banda la simba na jamaa ikatakiwa aingie ndani ya banda hilo,watalii walivofika jamaa akaanza kujirusha kwa nguvu zote kama sokwe ili kuwafurahisha watalii,kwa bahati mbaya mbao zilizokuwa zinatenganisha kati ya simba na banda lake zikavunjika na jamaa aadumbukia ndani ya banda la simba.Kwa uoga jamaa akaanza kupiga kelele za kuomba msaada kwamba yeye ni binadamu,kwa mshangao akaona simba akimziba mdomo kisha akamwambia " oya mbona unakuwa muoga ivo?, hebu tulia sisi sio simba ni binadamu kama wewe."